Kipindi chapili dakika ya 56 Thomas Müller akaipatia bao la pili na kisha bao la tatu likafungwa na Arjen Robben dakika ya 59 na kufanya mtanange uwe ngumu kwa kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini na kikosi chake alichopanga leo.
Mlinda lango wa City Joe Hart amelaumiwa kwa kuchangia katika mabao ya Bayern. Kwanza akikosa kuokoa mkwaju kutoka masafa ya mbali wa Franck Ribery na pia kufungwa kwa urahisi na Arjen Robben bao la tatu liliothibitisha ushindi uliostahili kwa kikosi cha Pep Guardiola.
Thomas Muller alifunga bao la pili la Bayern. Mchezaji wa akiba Alvaro Negredo aliipatia City bao la kufuta machozi la City.
Beki wa zamani wa City Jerome Boateng alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumpiga mueleka Yaya Toure wakati City ikiimarisha mashambulizi ambayo hayakufua dafu.
Frank Ribery na Micah Richards wote wakikimbilia mpira...
Muuaji wa bao la mwisho la tatu Arjen Robben
Patashika kwenye eneo la hatari la box
Bosi wa City Manuel Pellegrini akipagawa kwa kichapo na kuwalalamikia wachezaji wake kutobweteka
Mchezaji wa Manchester City Yaya Toure akimkaba vilivyo Toni Kroos wa Bayern
Muller akimfanyia sitaki nataka kipa Joe Hart na kumchomoa mpira na kufunga
Hapa ndipo raha ya ushindi inaanzia, Meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola akishangilia bao la mwisho la tatu kwa aina yake...
Alvaro Negredo akifunga bao la kufutia machozi na kufanya 3-1
Mashabiki wa Bayern wakipeperusha scarfs juu kwenye uwanja wa Etihad usiku wa leo
RATIBA/MATOKEO
Jumatano 2 Oktoba 2013
Shakhtar Donetsk 1 v 1 Manchester United FC
Bayer 04 Leverkusen 2 v 1 Real Sociedad de Fútbol
Juventus 2 v 2 Galatasaray A.Ş.
Real Madrid 4 v 0 København
Paris Saint-Germain 3 v 0 SL Benfica
RSC Anderlecht 0 v 3 Olympiacos FC
Manchester City 1 v 3 Bayern München
PFC CSKA Moskva 3 v 2 Viktoria Plzeň
No comments:
Post a Comment