KLABU ya Yanga, yenye maskani yake Mtaa wa Jangwani, jijini Dar es Salaam, imepanga kuuita ‘Jangwani City’, uwanja wake unaotarajiwa kujengwa, ambapo wanaamini utapunguza adha kwa wakazi wa eneo hilo, kwenda mbali kufuata huduma za kijamii.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo, ambaye pia ni msimamizi wa Uwanja huo, Francis Kifukwe, alisema hivi sasa ujenzi umesimama na wanasubiria majibu ya maombi yao ya kuongezewa eneo na Manispaa ya Ilala pamoja na Wizara ya Ujenzi.
“Uwanja unatarajiwa kuchukua watu 40,000, ukiwa na hosteli, Kituo cha Mafunzo ya Vijana (Academy), viwanja vya mazoezi, sehemu ya kuegeshea magari, hoteli, ukumbi wa mikutano, ofisi mbalimbali, benki, zahanati, maduka, ukumbi wa sinema, ‘supermarket’ na sehemu ya kupumzika.
“Kutokana na mahitaji hayo na eneo lilivyo, waliona halitoshi, hivyo kuamua kuiomba Serikali eneo la ziada, kwa barua yenye kumbukumbu namba YASC/ARDHI/MWK/YM/46/2012 na YASC/ARDHI/MWK/YM/47/2012, ambapo kipindi cha mafuriko Serikali iliwahamisha wakazi wa eneo hilo,” alisema Kifukwe.
Alisema, walishaongea na Mkuu wa Mkoa, Said Mecky Sadick, kwa ajili ya kuwasaidia katika suala hilo, ambapo hadi hivi sasa wanasubiri majibu, ndipo waanze ujenzi huo waliousitisha.
Mwaka jana, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alithibitisha kuwa mwisho wa eneo linaloruhusiwa kwa ujenzi ni unapoishia Uwanja wa Kaunda, ambao unamikiwa na Yanga na kwamba nyumba na watu wengine waishio nje ya eneo hilo hawapo kihalali.
Tibaijuka alisema kuwa makazi ya watu kwenye eneo hilo yangeweza kubomolewa wakati wowote, kutokana na kwamba eneo hilo la Jangwani halikuwa salama kwa makazi ya binadamu.
Yanga tayari imeshafanya mazungumzo na Kampuni ya Beijing Construction kutoka nchini China, iliyohusika kujenga Uwanja wa Taifa, kwa ajili ya ujenzi na kuchagua ramani ya uwanja wao, ambao utakuwa katika hadhi ya kimataifa.

No comments:
Post a Comment