BUKOBA SPORTS

Monday, October 14, 2013

WACHEZAJI ENGLAND WAWAPANIA POLAND, KOCHA NAE HODGSON ATAKA USHINDI KIVYOVYOTE!!

Roy Hodgson ametoa ahadi kwamba England haitabweteka ila itatafuta ushindi watakapocheza na Poland Jumanne Usiku Uwanjani Wembley katika Mechi ya mwisho ya Kundi H la Kombe la Dunia ambapo wakishinda tu watatinga Brazil Mwakani.
England wanaongoza Kundi H wakiwa Pointi 1 mbele ya Ukraine ambao wanamaliza na ‘vibonde’ San Marino.

Hodgson amesema Wachezaji wake wanajua kazi yao haijamalizika na inabidi waifunge Poland ambayo imeshapoteza nafasi ya kwenda Brazil na inacheza kukamilsha Ratiba tu.

Hata hivyo, Wachambuaji wa Soka wamekumbusha yaliyowakuta England Mwaka 1973 waliposhindwa kuifunga Poland na pia walipofungwa na Croatia Mwaka 2007 Uwanjani Wembley na kuikosa nafasi ya kucheza Fainali za EURO 2008.

Baada ya kuwapoteza Wachezaji wawili, Tom Cleverley, ambae ni Majeruhi na Kyle Walker, ambae amefungiwa baada ya Kadi za Njano, Roy Hodgson amemwita kwenye Kikosi chake Chipukizi Raheem Sterling wa Liverpool.
Ingawa Poland wanacheza Mechi hii na England kukamilisha Ratiba tu, Uwanja wa Wembley unategemewa kuwapokea Washabiki 18,000 wa Poland watakaokwenda kushangilia Timu yao.


Chini ya Kanuni za UEFA, Poland walitakiwa wapewe Tiketi 9,000 tu kwa vile Mgao wao ni Asilimia 10 ya Uwanja, na Wembley inachukua Watu 90,000, lakini FA iliamua kuwapa Tiketi 18,000.
RATIBA-KUNDI H:

Jumanne Oktoba 15

[Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku]

England v Poland

Montenegro v Moldova

San Marino v Ukraine

MSIMAMO:
KUNDI H










NAFASI Team P W D L F A GD Pts

1 England 9 5 4 0 29 4 25 19

3 Ukraine 9 5 3 1 20 4 16 18

2 Montenegro 9 4 3 2 16 12 4 15

4 Poland 9 3 4 2 18 10 8 13

5 Moldova 9 2 2 5 7 15 -8 8

6 San Marino 9 0 0 9 1 46 -45 0





















No comments:

Post a Comment