BUKOBA SPORTS

Saturday, November 16, 2013

NIGERIA WA KWANZA KULIONA LANGO LA BRAZIL 2014, BAADA YA KUIFUNGA ETHIOPIA BAO 2-0 MUUAJI AKIWA VICTOR MOSES NA VICTOR OBINNA!!

MABINGWA wa Afrika, Nigeria, leo huko kwao UJ Esuene Stadium Mjini Calabar, wameichapa Ethiopia Bao 2-0 na kuwa Nchi ya kwanza toka Bara la Afrika kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani.
Afrika inazo Nafasi 5 kwenye Fainali za Kombe la Dunia na nyingine zitaamuliwa baada ya Mechi nyingine 4 za Marudiano za Raundi ya Mwisho ambazo zinaendelea leo, kesho na Jumanne.

Nigeria, ambao waliifunga Ethiopia Bao 2-1 huko Addis Ababa katika Mechi ya kwanza Mwezi Oktoba, walifunga kupitia Victor Moses, Penati ya Dakika ya 20, na Mchezaji alietoka Benchi, Victor Obinna, kwa frikiki ya Dakika ya 83.

Hii itakuwa mara ya 5 kwa Nigeria kucheza Fainali za Kombe la Dunia.

We're going to Brazil! A shirtless Victor Moses celebrates after scoring Nigeria's opening goal from the penalty spot
Tunaenda Brazil !!! Mchezaji Victor Moses akishangilia huku akiwa amevua jezi kifua wazi baada ya kufunga penati na kuipatia bao la kuongoza kipindi cha kwanza Nigeria
Patashika kuusaka mpira hapa!!
On the attack: Chelsea's Mikel John Obi takes the ball ahead of Ethiopia's Adane Girma (left) and Shemeles Bekele (right) during the match in Calabar
Mchezaji wa Chelsea na timu ya Taifa ya Nigeria Mikel John Obi takibanwa na wachezaji wa Ethiopia Adane Girma (kushoto) na Shemeles Bekele (kulia) leo huko Calabar
Hottest ticket in town: Supporters arrive for the second leg with a World Cup place at stake
Tunataka kuwaona wenzetu kaka zetu Mastaa wetu !!! Mashabiki wa Nigeria wakikaguliwa na askari mlangoni wakati wa kuingia uwanjani leo huko Calabar Nigeria.
VIKOSI:
Nigeria: Enyeama, Ambrose, Oboabona, Elderson, Omeruo (Egwueke 68), Brown (Mba 59), Moses (Obinna 79), Onazi, Mikel Obi, Musa, Emenike
Substitutes not used: Ejide, Reuben, Oduamadi, Ogu, Dike, Agbim, Okwuosa
Scorer: Moses 20 (penalty), Obinna 83
Booked: Moses, Omeruo

Ethiopia: Bancha, Girma, Abebaw, Bareghizo, Hailu, Minyahile (Fekadu 81), Bekele (Hintsa 75), Kebede (Assefa 60), Girma, Gubena, Said Ahmed
Substitutes not used: Debebe, Bogale, Biadigling, Tassew, Jemes, Tadese, Aspaw
Booked: Girma, Said Ahmed, Bareghizo
Referee: Bakary Papa Gassama (Gambia)

No comments:

Post a Comment