MANCHESTER City imeifumua mabao 4-2 Viktoria Plzen Uwanja wa Etihad usiku huu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mabao ya City yamefungwa na Aguero kwa penalti dakika ya 33, Nasri dkika ya 65, Negredo dakika ya 79 na Dzeko dakika ya 90, wakati mabao ya Viktoria Plzen yamefungwa na Horava dakika ya 43 na Tecl dakika ya 69.
Wachezaji wakiingia uwanjani tayari kuanza mchezo.
Manchester City, ambao tayari walikuwa wamefuzu kabla ya Mechi hii, wameitwanga Plzen Bao 4-2 katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Etihad.
Bao za City zilifungwa na Agüero, kwa Penati, Nasri, Negredo na Dzeko huku Bao za Plzen zikifungwa na Horava na Tecl.
Kikosi cha City cha kwanza kikijipanga kupata picha

Kipa wa City Joe Hart akiruka juu kuokoa mpira

Sergio Aguero akituma vitu kwenye lango la Plzen

Hart akiruka kuokoa mpira hapa kwenye lango lake

Samir akifunga bao na kufanya 2-1 dhidi ya Plzen

Wachezaji wa City wakipongezana baada ya kupata bao

Wachezaji wa City wakimkaba mchezaji wa Plsen

Mashabiki wa Plzen wakishangilia

Alvaro Negredo akifanya 3-2...

Edin Dzeko akifunika baada ya kumaliza bao la mwisho la nne na kufanya mtanange umalize dakika 90 bao zikiwa 4-2.
No comments:
Post a Comment