Meneja David Moyes amethibitisha kukosekana kwao na wote hawakuwemo kwenye Kikosi kilichosafiri leo kutoka Jiji la Manchester kwenda huko Germany.
Licha ya Vidic kufanya Mazoezi Asubuhi hii, Moyes amesema: “Wote bado wana maumivu. Wote si maumivu ya muda mrefu lakini hawapo tayari kwa sasa.”
Hata hivyo, Man United itafarijika kwa kurudi tena Kikosini kwa ‘kiraka’ Phil Jones ambae alikuwa nje kwa maumivu ya nyonga lakini itawakosa Michael Carrick, ambae ni Majeruhi, na Marouane Fellaini, ambae yupo Kifungoni kwa Mechi moja baada ya Kadi Nyekundu katika Mechi iliyopita ya Kundi A la UCL walipotoka Sare na Real Sociedad huko Spain.
Hii ni Mechi ngumu kwenye Kundi A ambayo Mshindi wake ndie atakaefuzu kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ingawa kwa Man United hata Sare kwao si mbaya.
Wakiwa kwao BayArena Msimu huu, Bayer Leverkusen wameshinda Mechi zao zote kasoro moja dhidi ya Mabingwa wa Germany na Ulaya, Bayern Munich, ambayo walitoka Sare.
Baadhi ya wachezaji wa United wakifanya mazoezi kabla ya kuelekea Ujerumani
Giggs akiwekwa kati kwenye mazoezi leo!
Meneja wa United David Moyes anasongwa na wachezaji kadhaa ambao ni majeruhi.
Marouane Fellaini kwenye mazoezi leo hii huku Michael Carrick akiwa anasongwa na majeraha aliyoyapata hivi karibuni.
Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa Old Trafford Mwezi Septemba, Man United iliifunga Bayer Leverkusen Bao 4-2.
Katika Mechi ya leo, Man United wanahitaji ushindi ili wafuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL lakini pia hata Sare itawafanikisha.Vile vile, Uwanjani kwao BayArena hawafungiki na mara ya mwisho kufungwa ni Mwezi walipofungwa na Mabingwa Bayern Munich.
KUNDI A | |||||||||
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Manchester United | 4 | 2 | 2 | 0 | 6 | 3 | 3 | 8 |
2 | Bayer 04 Leverkusen | 4 | 2 | 1 | 1 | 8 | 5 | 3 | 7 |
3 | FC Shakhtar Donetsk | 4 | 1 | 2 | 1 | 3 | 5 | -2 | 5 |
4 | Real Sociedad | 4 | 0 | 1 | 3 | 1 | 5 | -4 | 1 |
No comments:
Post a Comment