Cameroon wakicheza huko Stade Omnisport Ahmadou Ahidjo -Yaoundé leo kwenye marudiano wameifunga Tunisia Bao 4-1, Mabao ya Cameroon yamefungwa kipindi cha kwanza na cha pili, Mchezaji P. Webó akiwafungulia Cameroon bao la kwanza katika dakika ya 4, Moukandjo Bile akifunga bao la pili dakika ya 30, Huku Jean Makoun akimalizia bao mbili peke yake dakika ya 65 na 86.
Bao la Tunisia limefungwa na mchezaji Ahmed Akaïchi dakika ya 51 kipindi cha pili. Katika mchezo wa raundi ya kwanza Cameroon v Tunisia walitoshana nguvu ya bila kufungana na kutoka 0-0, Ushindi huu wa marudiano unafanya jumla ya idadi ya mabao kuwa 4-1.
Ushindi huu wa Cameroon unawaunganisha na Nigeria pamoja na Ivory Coast ambao wameishajikatia tiketi ya kucheza kombe la Dunia huko Brazil mwakani 2014.Hii ni mara ya 6 kwa Cameroun kucheza Fainali za Kombe la Dunia na mara nyingine zikiwa Miaka ya 1982, 1990, 1994, 1998, 2002 na 2010 ambayo ni Rekodi kwa Afrika.
RATIBA:
Jumanne Novemba 19
19:00 Egypt v Ghana (1-6)
21:15 Algeria v Burkina Faso (2-3)
No comments:
Post a Comment