BUKOBA SPORTS

Sunday, December 1, 2013

EMMANUEL MSUYA AIBUKA MSHINDI WA EBSS 2013


Mshindi wa Epiq Bongo Star Search 2013, Emmanuel Msuya (kati) akishukuru Mungu baada ya kutangazwa kushinda zawadi ya milioni 50 za shindano hilo lililodhaminiwa na Zantel. Kulia ni mshindi wa pili, Elizabeth Mwakijambile na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Zantel, Ali Bakari.

Msuya akiangua kilio cha furaha baada ya kutangazwa mshindi.

Msuya akiangua kilio cha furaha baada ya kutangazwa mshindi.

Amina Chibaba, Elizabeth Mwakijambile, Maina Thadei na Melisa John.

Maina Thadei.

Walioingia tatu bora.(picha zote na habari na Francis Dande)

Mshindi wa Epiq Bongo Star Search, Emmanuel Msuya akiwa na mshindi wa pili wa shindano hilo, Elizabeth Mwakijambile kabla ya kutangazwa kwa mshindi wa shindano hilo.

Mshindi wa pili wa shindano la Epiq Bongo Star Search, Elizabeth Mwakijambile akiwajibika jukwaani.



Emmanue Msuya.

Amina Chibaba.

Mshindi washindano la Epiq Bongo Star Search, Emmanel Msuya akiwajibika jukwaani.

Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search, Emmanuel Msuya wa jijini Mwanza (katikati), akipokea kitita cha sh. milioni 50 kutoka kwa jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen baada ya kuwashinda washiriki wenzake watano walioingia katika fainali hizo. Wa pili kulia ni Ofisa Mkuu wa Fedha wa Zantel, Ali Bakari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel

Mashabiki wakifuatilia fainali hizo.

Majaji.

Emmanuel Msuya.

Wasanii wakitoa burudani.

Barnabas Elias 'Barnaba' wa THT akitumbuiza.

Melisa John.

Emmanuel Msuya.

Na Elizabeth John
Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja.
Emmanuel Msuya wa jijini Mwanza, jana usiku aliibuka mshindi wa Epiq Bongo Star Search (EBSS) kwa mwaka huu baada ya kuwabwaga wengine wanne waliofika hatua ya fainali, hivyo kutwaa kitita cha shilingi milioni 50.
Msuya aliibuka kidedea katika fainali hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Escape One uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam na kupambwa na wasanii mbalimbali wakiongozwa na mkali kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania (THT), Elias Barnaba ‘Barnaba Boy’.
Mbali na kuondoka na fedha hizo, Msuya atapata mkataba wa kurekodi nyimbo zake katika studio ya MJ rekodi inayomilikiwa na Jaji wa mashindano hayo, Joachim Kimario ‘Master Jay’ pamoja na kukatiwa bima ya afya ya kutibiwa mwaka mzima.
Msuya aliwabwaga washiriki wengine walioingia fainali, Amina Chibaba, Elizabeth Mwakijambile, Maina Thadei na Melisa John.
Nyota huyo aliibuka kidedea baada ya kuimba kibao cha ‘Maneno maneno’ kilichoimbwa na mkali wa muziki wa RnB nchini, Bernard Paul ‘Ben Pol’ ambapo pia mshindi wa mwaka jana, Walter Chilambo aliondoka na kitita hicho baada ya kuimba wimbo wa msanii huyo unaojulikana kwa jina la ‘Nikikupata’.

Jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen ‘Madam Ritha’ alisema ili mshiriki aweze kuibuka mshindi anatakiwa kujiamini anapokuwa jukwaani na kuweza kulimiliki jukwaa vizuri.
“Vigezo tunavyoangalia kumpa ushindi, mshiriki anatakiwa kuwa na imani na anachokifanya, umahiri wake wa kuimba anapokuwa jukwaani, pia huwa tunamshauri mshiriki kuimba wimbo ambao anaufahamu vizuri,” alisema Madam Ritha.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Msuya alisema yeye hajui ni kitu gani kimempa ushindi huo yote anamuachia mungu.
“Kiukweli siwezi kuzungumza lolote kwani nina furaha ya ajabu, mimi sijui lolote najua mungu alikuwa na mimi pia nawashukuru sana majaji wangu pamoja na Watanzania wote ambao walikuwa wananipigia kura,” alisema.

Mbali na Barnaba, wasanii wengine waliopamba fainali hizo ni pamoja na msanii chipukizi wa hip hop, Kimbunga, Young Killer ‘Msodoki’, Makomandoo, Snura na Shaa.
Shindano hilo kwa mwaka huu limedhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Zantel pamoja na Salama Kondomu.

No comments:

Post a Comment