BUKOBA SPORTS

Monday, December 16, 2013

EUROPA LEAGUE: RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 32 HIYOO...PAMOJA NA DROO YA RAUNDI YA TIMU 16 YAFANYIKA LEO. SWANSEA v NAPOLI, DNIPRO v TOTTENHAM..JUVENTUS v TRABZONSPOR....

LEO huko Nyon, Uswisi imefanyika Droo ya EUROPA LEAGUE ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 pamoja na ile ya Raundi inayofuata ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16. Swansea wamepangiwa kucheza na Napoli ya Italy wakati Tottenham, ambao walijikuta hawana Meneja Dakika chache kabla ya Droo hii baada kufukuzwa kazi Andre Villas-Boas, watacheza na Dnipro ya Ukraine.
Kwa sasa Dnipro iko chini ya Kocha wa zamani wa Tottenham, Juande Ramos.

Kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Swansea na Tottenham, zote zinaweza kukutana na Klabu kutoka Ureno ikiwa zote zitafuzu kwa Swansea, ikiwa wataitoa Napoli, kucheza na Mshindi kati ya Porto au Eintracht Frankfurt na Tottenham, ikiwa wataifunga Dnipro, kupambana na Benfica au Klabu ya Ugiriki, PAOK.
DROO KAMILI:RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 32:
{Mechi za kwanza kuchezwa Februari 20 na Marudiano Februari 27}
Dnipro v Tottenham
Real Betis v Rubin Kazan
Swansea v Napoli
Juventus v Trabzonspor
Maribor v Sevilla
Plzen v Shakhtar Donetsk
Chornomorets Odesa v Lyon
Lazio v Ludogorets
Esbjerg v Fiorentina
Ajax v Salzburg
Maccabi Tel Aviv v Basel
Porto v Eintracht Frankfurt
Anzhi v Genk
Dynamo Kiev v Valencia
PAOK v Benfica
Slovan Liberec v AZ

RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16:
[Mechi za kwanza kuchezwa Machi 13 na Marudiano Machi 20]
Liberec/AZ v Anzhi/Genk
Lazio/Ludogorets v Dynamo Kiev/Valencia
Porto/Frankfurt v Swansea/Napoli
Odesa/Lyon v Plzen/Shakhtar
Maribor/Sevilla v Real Betis/Rubin Kazan
Dnipro/Tottenham v PAOK/Benfica
Maccabi/Basel v Ajax/Salzburg
Juventus/Trabzonspor v Esbjerg/Fiorentina

No comments:

Post a Comment