BUKOBA SPORTS

Monday, December 9, 2013

MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANZANIA YAFANA SANA LEO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kulia akizunguka uwanja huku akiwa anawasalimia Wananchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) mbele


Taswira





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga 21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.

Sehemu ya askari wa vikosi vya ulinzi na usalama wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wakati kabla ya kamanda wa gwaride kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kukagua gwaride hilo leo jijini Dar es salaam.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akiwasili jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo.

Gwaride likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mwendo wa haraka.

Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakati gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalama likipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa haraka.

Baadhi ya Maofisa wa jeshi wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam. Picha na 9.Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam waliojitokeza kuhudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.

Wananchi wakifatilia

Vijana wa halaiki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakitamka kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es salaam ambayo ni “ Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu,Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ta Taifa Letu”.

Vijana wa halaiki wakiendelea kuwasilisha jumbe mbalimbali kama inavyoonekana mfano wa mnyama aina ya samba kuashiria utalii katika hifadhi za wanyama za Tanzania.

Vijana wa halaiki wakionyesha ukakamavu.

Baadhi ya Maafisha wa Jeshi wakitoa salamu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hatuba fupi kwa watanzania wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Hatuba yake licha ya kujaa maneno ya kumkumbuka rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Rolihlahla Mandela Madiba aliyeaga dunia juzi nchini Afrika ya Kusini imesisitiza Upendo, Amani, Mshikamano miongoni mwa watanzania na kukemea tabia ya baadhi ya viongozi kulipiza kisasi pindi waingiapo madarakani.

Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo katika uwanja wa Uhuru wakati wa Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.

Raia wa kigeni waliohudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.

Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange alipokua akisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO

No comments:

Post a Comment