Wanachama wa chama tawala nchini Afrika Kusini ANC hii leo wanapata fursa ya kuuaga mwili wa Rais wa kwanza mzalendo wa Taifa hilo Nelson Mandela aliyefariki dunia juma tarehe 5 Desemba jijini Johannesburg. ANC wanapata nafasi hiyo baada ya kutamatika kwa siku tatu za kutoa heshima za mwisho katika majengo ya serikali ambapo takribani watu laki moja walipata nafasi ya kuuaha mwili wa kiongozi huyo.
Wananchi wengi walitamani kutoa heshima za mwisho na hata kukesha eneo hilo lakini wengine walikosa nafasi kutokana na umati kuwa mkubwa zaidi.Mwili wa Hayati Madiba utapelekwa kijijini kwake Qunu hii leo tayari kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika hapo kesho jumapili.
Wakati huo huo serikali ya Afrika Kusini imesema inachunguza ili kubaini waliohusika kumuajiri Mkalimani wa lugha za alama ambaye alilalamikiwa kupotosha kwa kutumia ishara zisizo sahihi katika kumbukumbu ya kumuenzi Mandela iliyofanyika siku ya jumanne.
Mkalimani huyo Thamsanqa Jantjie alitumika kutafrisi hotuba za viongozi mbalimbali wa dunia akiwemo Rais wa Marekani Barack Obama.
Hivi karibuni mtu huyo alijitokeza mbele ya wanahabari na kuomba radhi kuwa hakufanya kazi yake kwa umahiri kutokana na kukabiliwa na maradhi lakini yeye ni mtaalamu wa kazi hiyo.
Kituo kimoja cha Televisheni cha binafsi nchini humo cha eNCA kimeripoti kuwa mtu huyo amewahi kukabiliwa na mashtaka ya jinai yakiwemo mauaji na utekaji.Msemaji wa serikali Phumla Williams amesema serikali inachunguza iwapo makosa ya kiusalama yalifanyika hadi Jantjie akapewa pasi za usalama.
Snub: Xhosa youths are pictures in Qunu ahead of the funeral of Nelson Mandela
Tradition: Locals in Qunu slaughter six sheep in preparation for a memorial service for Nelson Mandela in his birth village
No comments:
Post a Comment