BUKOBA SPORTS

Friday, December 13, 2013

PENGO KWA UNITED! ROBIN VAN PERSIE NJE MWEZI MMOJA!

Mchezaji Straika wa Manchester United Robin van Persie atakuwa nje ya Uwanja kwa Mwezi mmoja akijiuguza tatizo la Paja.
Van Persie, Miaka 30, alijiumiza wakati akipiga Kona ambayo Phil Jones alifunga Bao la ushindi hapo Jumanne Uwanjani Old Trafford wakati Man United inaifunga Shakhtar Donetsk Bao 1-0 kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONS.

Akiongelea habari hizi hii leo, Meneja wa Man United, David Moyes, amesema: “Ni bahati mbaya. Rekodi yetu ni nzuri wakiwepo Wayne Rooney na Robin kwenye Timu. Hatujakuwa nao pamoja kitambo sasa. ”

Msimu huu, Van Persie amekuwa akikumbwa na majeruhi kadhaa yakiwemo kuumia Kidole cha Mguu na Nyonga na Wikiendi iliyopita alirejea Uwanjani baada Mwezi mmoja nje akitokea Benchi kwenye Mechi Man United waliyofungwa 1-0 na Newcastle.
Vasn Persie alitua Old Trafford Agosti 2012 akitokea Arsenal kwa Dau la Pauni Milioni 24 na kufunga Bao 26 katika Msimu wake wa kwanza na kuisaidia Man United kutwaa Taji la Ubingwa la 20.


Robin van Persie na takeaway mkononi huko Alderley Edge jumatano

Van Persie alichukua msosi wa mchana na kusepa zake..ambapo habari za kuumia paja zimezungumziwa rasmi leo na Kocha mkuu David Moyes.

Van Persie aliingia uwanjani dakika ya 63dhidi ya Shakhtar Donetsk jumanne juzi.

Habari mbaya kwa David Moyes ...na safari hii wakiwa na mchezo ugenini na Aston Villa jumapili kesho kutwa.

MITANANGE 8 ATAKAYOKOSA ROBIN VAN PERSIE
Aston Villa (A), Dec 15, Premier League
Stoke (A), Dec 18, League Cup
West Ham (H), Dec 21, Premier League
Hull (A), Dec 26, Premier League
Norwich (A), Dec 28, Premier League
Tottenham (H), Jan 1, Premier League
Swansea (H), Jan 5, FA Cup
Swansea (H), Jan 11, Premier League

No comments:

Post a Comment