KIUNGO mahiri wa klabu ya Barcelona, Cesc Fabregas amemtaja meneja wa Arsenal, Arsene Wenger kuwa mtu muhimu katika kazi yake ya soka. Fabregas mwenye umri wa miaka 26 alisajiliwa na Wenger kutoka katika timu ya vijana ya Barcelona akiwa na umri wa miaka 16 na haraka alionyesha kiwango kizuri katika timu ya vijana ya Arsenal kabla ya kucheza kwa mara ya kwanza timu ya wakubwa mwaka 2003. Kwa ujumla Fabregas amecheza Arsenal kwa miaka nane kabla ya kurejea Camp Noun na ingawa alifanyiwa kunyakuwa taji la FA pekee mwaka 2005 bado anadhani kocha huyo ni muhimu kwake. Wakati huohuo Fabregas sambamba na Wenger walimtetea kiungo Mezut Ozil ambaye mashabiki wamekuwa wakihoji juu ya kiwango chake kuporomoka hivi karibuni. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani ameshindwa kufunga bao katika mechi nane zilizopita za timu hiyo huku akishindwa kutengenza nafasi hata moja iliyozaa bao toka Desemba mwaka jana. Hata hivyo Wenger pamoja na Fabregas wamedai kuwa Ozil anajitahidi kuzoea mazingira ya Ligi Kuu nchini Uingereza anachohitaji ni muda kabla hajarudisha makali yake.SARE YAMPA AHUENI WENGER.
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa kikosi chake kingeweza kuondoka na alama zote tatu dhidi ya Manchester United jana lakini ameridhishwa na jinsi safu yake ya ulinzi ilivyocheza baada ya kipigo cha kudhalilisha walichokipata kutoka kwa Liverpool wiki iliyopita. Sare ya bila kufungana waliyopata dhidi ya United jana iliinyima nafasi timu hiyo kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza hivyo kuwaacha Chelsea wakiendelea kujitanua huko juu. Akihojiwa kuhusiana na mechi hiyo ya jana, Wenger amesema anadhani walikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwani walipoteza baadhi ya nafasi chache muhimu walizotengeneza. Wenger aliendelea kudai kuwa anawapongeza mabeki wake kwani walifanya kazi kubwa ya kutorudia makosa waliyofanya katika mchezo dhidi ya Liverpool Jumamosi iliyopita. Arsenal bado wako katika mwezi mgumu kwani Jumamosi wanatarajiwa kuikaribisha Liverpool katika mchezo wa Kombe la FA kabla ya kuwakaribisha mabingwa wa Ulaya Bayern Munich katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani humo siku tatu baadae.
No comments:
Post a Comment