Mchezaji matata Emmanuel Adebayor akishangilia bao lake katika dakika ya 65 kipindi cha pili dhidi ya Everton, Ambapo mtanange huo umemalizika kwa bao 1-0.
Adebayor akiachia shuti kali mbele ya Kyle Walker na kumfunga kipa wa Everton Tim Howard na kufanya 1-0 dhidi ya Everton.
Meneja wa England Roy Hodgson nae alikuwemo uwanjani White Hart Lane kucheki mtanange huo
Kipa wa Everton Tim Howard akiokoa mpira mbele ya Emmanuel Adebayor katika kipindi cha pili.
Meneja wa Everton Roberto Martinez na Meneja wa Muda wa Tottenham Tim Sherwood wakiwa ndani ya mstari kusaka pointi muhimu na kusimamia wachezaji wao leo kwenye uwanja wa White Hart Lane kwenye matanange wa Ligi kuu England. Spurs wameshinda bao 1-0 dhidi ya Everton waliokuwa ugenini.
No comments:
Post a Comment