BUKOBA SPORTS

Monday, February 3, 2014

USIKU HUU NI PATASHIKA!!! - EPL: MANCHESTER CIY v CHELSEA, REFA NI MIKE DEAN.


Usiku huu, Manchester City, ambao wako Nafasi ya Pili Pointi 2 nyuma ya Arsenal, na Chelsea walio Nafasi ya 3, Pointi 3 nyuma ya Man City, wanakutana kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ambayo matokeo yake yatafafanua zaidi nini kitajiri mbio za Ubingwa Msimu huu.
Mwamuzi wa mtanange wa leo ni Mike Dean Wote wawili wanatafuta nafasi ya kulitwaa kombe la msimu huu 2013/2014
Hii ni Mechi ya Pili kukutana Msimu huu na katika Mechi ya Kwanza huko Stamford Bridge, Chelsea waliibuka kidedea kwa Bao 2-1. Kwenye Mechi hii, Timu zote zitawakosa Mastraika wao hatari, Sergio Agüero na Fernando Torres, ambao waliziona nyavu walipokutana Stamford Bridge mapema mwanzoni mwa Msimu huu.Aguero na Torres watauangalizia nje mpira huu.Jembe jipya: Mohamed Salah anaweza akacheza katika mtanange huu?VIKOSI VINATARAJIWA KUWA HIVI:
Man City (Possible, 4-2-3-1): Hart; Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy; Fernandinho, Touré; Silva, Jovetic, Navas; Negredo.
NJE: Agüero (hamstring), Milner (groin), Nasri (knee), Javi Garcia (unspecified)
Chelsea (Possible, 4-2-3-1): Cech; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Ramires, Lampard; Willian, Oscar, Hazard; Eto'o. NJE: Torres, Van Ginkel (knee).

No comments:

Post a Comment