BUKOBA SPORTS

Monday, June 9, 2014

CLARENCE SEEDORF KIBARUA CHAOTA NYASI, ATIMULIWA AC MILAN, FILIPPO INZAGHI ACHUKUWA MIKOBA YAKE

Relieved of his duties: Clarence Seedorf has been sacked as manager of AC Milan
AC Milan imemtimua Kocha wao Clarence Seedorf na kumbadili na Filippo Inzaghi.
Seedorf alichukua hatamu huko San Siro Mwezi Januari na kumbadili Massimiliano Allegri wakati huo Wakongwe hao wa Soka huko Italia wakiselelea katikati ya Msimamo wa Ligi ya Serie A.
Hata hivyo, Seedorf alimudu kushinda Mechi zake 11 za Ligi kati ya 19 na kuiwezesha AC Milan kumaliza Nafasi ya 8 lakini ikakosa hata Nafasi ya kucheza EUROPA LIGI.
Licha ya mafanikio kidogo chini ya Seedorf ukilinganisha na Massimiliano Allegri, Leo hii AC Milan imetangaza kumwondoa na nafasi yake kupewa Inzaghi ambae alicheza pamoja na Seedorf hapo hapo AC Milan.

Pointing the way: AC Milan legend Filippo Inzaghi has been appointed as the new manager at the San SiroAC Milan legend Filippo Inzaghi aliyechaguliwa kuchukua nafasi yake
Inzaghi amepewa Mkataba wa Miaka miwili.
Taarifa kwenye Tovuti ya AC Milan ilithibitisha kufukuzwa Seedorf na kuteuliwa Inzaghi ambae Mkataba wake utamalizika Juni 30, 2016.
Struggles: Milan, playing with Mario Balotelli up front, finished eighth in Serie A last seasonKabla ya uteuzi wa Leo, Inzaghi alikuwa Kocha wa Timu ya Vijana wa chini ya Miaka 19 ya AC Milan na jukumu lake kubwa hivi sasa ni kurudisha tena mafanikio ya Klabu hiyo ambayo iliwahi kuwa Mabingwa wa Ulaya mara 7. 
Akiwa Mchezaji wa AC Milan na pia Timu ya Taifa ya Italy, Inzaghi aliichezea Klabu hiyo Mechi 300 na kufunga Bao 126 na kutwaa Ubingwa wa Italy mara 2 na UEFA CHAMPIONZ LIGI mara 2 katika Miaka yake 11 ya Uchezaji.
Nafasi ya 8 waliyomaliza AC Milan kwenye Serie A Msimu huu uliomalizika Majuzi ni ya chini kabisa tangu 1998 na wamemaliza wakiwa Pointi 55 nyuma ya Mabingwa Juventus.

No comments:

Post a Comment