Na Faustine Ruta, BukobaCOSAD Ni shirika lisilo la Kiserikali ambalo limezindua Miradi yake katika Manispaa ya Bukoba. Leo Jumanne limeendelea kupanua Wigo mpana wa Miradi yake katika Moja ya mradi wake wa Mbuzi wa Maziwa katika Vijiji vya Kangabusharo na Kitwe. Hafla fupi iliyoudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Cosad Tanzania Bw. Smart Baitani, Mratibu wa Miradi Nchini Brittany Leitch, Mshauri Mkuu wa Miradi ya (OWOG) Dr. Erasmus Emmanuel, Mwakilishi wa Ubarozi Mickie Donan na Wananchi wa Kitwe na Baadhi ya Watumishi wa COSAD Tanzania. COSAD na Wananchi wanashukuru Kanisa la Edina Lovenant Church hasa kwa Mchungaji Ben Swanson wa Minnesota, USA.
Dume la Mbuzi
Mbuzi wa Maziwa wanaofugwa na Cosad
Dr. Erasmus akiendelea kutoa maelezo kuhusu mbuzi hao wanaofungwa na Shirika hilo.
Mratibu wa Miradi Nchini Brittany Leitch akichukua picha kwa simu yake kwenye Shamba la Mradi wao wa Mbuzi.
Dada Plascovia kutoka Shirika la Cosad
Ubao wa Tangazo shamba la Mbuzi, ambapo Mbuzi hufugwa katika eneo hilo maalum lililotengwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali Cosad, Linalohudumia Jamii na kutoa Ajira kwa Wananchi wa Bukoba.
Mbuzi wa Maziwa wakiwa kwenye Shamba lao
Mratibu wa Miradi Nchini Brittany Leitch akiwa na Mkurugenzi wa COSAD Bw. Smart Baitani wakiangalia Mifugo leo kabla ya kwenda kwenye Kijiji cha Kangabusharo Kitwe kutekeleza na kuendesha moja ya malengo kwa kina Mama ambao Wataendelea na Ufungaji kijijini hapo kwenye Mradi wa (One Woman, One Goat).
Mbuzi wa Maziwa
Kulia ni Mshauri Mkuu wa Miradi ya (OWOG) Dr. Erasmus Emmanuel na Nyuma ni Mkurugenzi wa COSAD Bw. Smart Baitani wakiangalia Mifugo leo.
Moja ya Mtumishi kutoka Shirika la Cosad, Monica Paulo
Picha ya pamoja Mkurugenzi wa COSAD Bw. Smart Baitani, Dr. Erasmus, na Mratibu wa Miradi Nchini Brittany Leitch pamoja na Dokta wa Mifugo.
Mratibu wa Miradi Nchini Brittany Leitch (kulia) akifurahia baada ya kupokewa na moja ya Mama waliojumuika pamoja kwenye kikundi cha Ufugaji Mbuzi kupitia Mradi wa Cosad.
Karibuni Sana Kijijini Kangabusharo...karibu!!
Dada Brittany Leitch akisalimiana na Mama baada ya kufikia Kijijini
Mkurugenzi wa COSAD Bw. Smart Baitani (katikati) akifurahia baada ya kufika Kijijini Kangabusharo.
Wa Bukoba ni wa Bukoba!!! Mkurugenzi wa COSAD Bw. Smart Baitani alishindwa kujizuia akajikuta anaenda hewani kwa Ngoma safi iliyotumbuizwa na Kinamama Kitwe kama Kuwakaribisha Wageni wao kutoka Shirika lisilo la Kiserikali COSAD.
Furaha ikatawala!!.jpg&container=blogger&gadget=a&rewriteMime=image%2F*)
Dr. Erasmus Emmanuel akitoa mafunzo kwa ufupi juu ya Mbuzi hao wa Maziwa waliopewa Wakina Mama. Akiwafundisha Jinsi ya Kuwalisha Mbuzi Wa Maziwa.
Ni muhimu kufahamu kuwa chakula unachomlisha mbuzi wako ndicho kitakachotengeneza maziwa hivyo basi ni muhimu kuyafahamu haya:
Kumpa mbuzi chakula katika mahali palipo safi kwa sababu :
- Mbuzi hula kila aina ya chakula hivyo usiwaruhusu kula chakula kilicho na mchanga
- Hali hii huwazuia kuambukizwa minyoo wanaopatikana kwenye mchanga
Mbuzi wa maziwa kwa mara nyingi hufugiwa kwenye zero grazing hivyo basi kumbuka kuwatengezea mahali pa kulia chakula na kunywea maji ambapo panahitajika kuwa juu na mbali na nyumba za kulala ili wasikanyage, au kuchafua chakula.
Mkurugenzi wa COSAD Bw. Smart Baitani(katikati) akiendelea kutoa maelezo kwa Kundi hilo la Kina Mama wakati wa utoaji wa Mbuzi hao wa maziwa.
Wakina Mama wakiwa na Mbuzi zao baada ya kukabidhiwa leo na Viongozi wa Cosad kupitia mrad wao wa "One Woman, One Goat" leo kwenye Kijini cha Kangabusharo Bukoba Vijijini.Ufugaji huo wa Mbuzi utaweza kumpa mkulima nyama na maziwa kwa matumizi ya nyumbani na mapato kutokana na mauzo ya ziada. Mifugo pia ni chanzo cha samadi.
Mbuzi wa maziwa hummtolea mkulima maziwa ya kunywa na kuuza, Samadi ya kurutubuisha ardhi na mbuzi wenyewe wanaweza kuuzwa. Na kipato cha ziada,wakulima wanaweza kulipa ada za nyumbani; kuwapeleka watoto wao shuleni ama kuwekeza mara nyingine kwa shamba na biashara zingine.
Zawadii zilitolewa kutoka kwa Kubdi hilo la Kina Mama Wafugaji wa mbuzi.
No comments:
Post a Comment