Kepteni wa Manchester united Wayne rooney akishangilia bao lao la kujifunga wenyewe Arsenal
WAKICHEZA Ugenini huko Emirates na Difensi ya kuungaunga iliyoongozwa na Chris Smalling akisaidiwa na Chipukizi Tyler Blackett na Paddy McNair na Mawinga wawili, Valencia na Ashley Young, Man United walifanikiwa kuwatwanga Arsenal Bao 2-1 na kuchupa hadi Nafasi ya 4 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu.
Wakitumia Mfumo wa 3-4-1-2, Meneja wa Man United Louis van Gaal alifanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza wa Ugenini kwenye Ligi baada ya kupata Mabao kupitia Mchezaji wa Arsenal Kieran Gibbs aliejifunga mwenyewe na Kepteni Wayne Rooney baada ya kaunta ataki.
Bao la Arsenal lilifungwa na Olivier Giroud alieingizwa kutoka Benchi akirejea Uwanjani baada ya kukaa Miezi Mitatu nje akiuuguza Mguu wake uliovunjika.
Licha ya kuanza na Difensi dhaifu, Man United pia walipata balaa katika Dakika ya 16 wakati Fulbeki Luke Shaw alipoumia enka na kubadilishwa na Winga Ashley Young.
Kipindi cha kwanza kimeanza...Arsenal wanafanya mashambulizi ya hapa na pale...Olivier Giroud akipasha kabla ya Mtanange kuanza
No comments:
Post a Comment