CAPITAL ONE CUP: KUMEKUCHA LEO JUMANNE!! ROBO FAINALI, DERBY vs CHELSEA, SHEFFIELD vs SOUTHAMPTON
Kombe la Ligi, Capital One Cup leo Jumanne Usiku Desemba 16 litakuwa na Mechi mbili za Robo Fainali na Siku inayofuata Jumatano kumalizia Robo Fainali mbili.
Kwenye Robo Fainali za kwanza, Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, watakuwa Wageni wa wa Klabu ya Ligi ya Daraja la chini yake, Championship, Derby County Timu ambayo iko Nafasi ya 3 kwenye Ligi hiyo.
Mechi nyingine ya Robo Fainali ya Jumanne ni kati ya Sheffield United, inayocheza Daraja la Ligi 1 likiwa ni Daraja la chini ya Championship, ikicheza na Timu ya Ligi Kuu England, Southampton.
Siku inayofuata Jumatano, kwenye Robo Fainali nyingine, Liverpool watakuwa Wageni wa Bournemouth ambao ndio Vinara wa Daraja la Championship na Mechi nyingine ni ile pekee ya Timu za Ligi Kuu England itakayochezwa White Hart Lane Jijini London kati ya Tottenham Hotspur na Newcastle United.
Washindi wa Mechi hizi wanatinga moja kwa moja Nusu Fainali.
CAPITAL ONE CUP
ROBO FAINALI
Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
Jumanne Desemba 16
Derby vs Chelsea
Sheffield United vs Southampton
Jumatano Desemba 17
Tottenham vs Newcastle
Bournemouth vs Liverpool
No comments:
Post a Comment