Licha ya kuwa Kifungoni toka kwa FIFA kwa Madrisha Mawili ya Uhamisho kutochukua Wachezaji wapya, Barcelona iliomba Kibali maalum chini ya Kanuni za Shirikisho la Soka la Spain ili kumsaini mbadala wa Beki hiyo wa Kimataifa kutoka Belgium lakini wamepigwa nje na FIFA.
Kamati ya Nidhamu ya FIFA imetamka kuwa Adhabu yao haina kipengele cha Kibali Maalum.
FIFA iliwaadhibu Barcelona kwa kuvunja Sheria za Kimataifa za kusaini Wachezaji Chipukizi na Adhabu yao ya kutosaini Wachezaji wapya kwa Madrisha Mawili ya Uhamisho inaanzia Dirisha la Uhamisho la Januari.
Hata hivyo, hivi sasa Barcelona wanasubiri Rufaa yao waliyoiwasilisha CAS, Court of Arbitration for Sport, Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, ambayo itakata shauri lao baadae Mwezi huu.
Licha ya kuhukumiwa mapema Mwaka huu, FIFA ilisitisha Adhabu kwa Barcelona hadi Rufaa itakaposikilizwa na FIFA na hilo likatoa mwanya kwao kumsaini Vermaelen kwa Dau la Euro Milioni 19 lakini hadi Leo hajacheza hata Mechi kutokana na maumivu.
No comments:
Post a Comment