BUKOBA SPORTS

Saturday, December 13, 2014

LA LIGA: SARE YAWACHANGANYA BARCA!! WATOKA 0-0 NA GETAFE

Lionel Mesi hakufurahishwa na sare ya 0-0 dhidi ya Getafe
Barcelona wamepata pigo katika mbio zao za kuwakamata Vinara wa La Liga Real Madrid baada ya kutoka Sare 0-0 na Getafe.
Katika Kipindi cha Kwanza kama si uhodari wa Kipa wa Barca Claudio Bravo kuokoa Shuti la Angel Lafita basi Getafe wangekuwa mbele.
Kipindi cha Pili, Lionel Messi nusura aipe Barca Goli wakati Shuti lake la Frikiki kugonga mwamba.
Matokeo haya yamewaacha Barca wakiwa Nafasi ya Pili Pointi 4 nyuma ya Vinara Real huku Mabingwa Watetezi Atletico Madrid wakiwa Pointi 3 nyuma ya Barca.
Mpaka mpira unamalizika dakika 90 ni 0-0.

No comments:

Post a Comment