BUKOBA SPORTS

Sunday, December 14, 2014

LIGI KUU ENGLAND 2014-15 (RATIBA, MSIMAMO, WAFUNGAJI NA UCHAMBUZI. MAN UNITED vs LIVERPOOL USO KWA USO LEO HII JUMAPILI!

WAFUNGAJI WA MABAO WANAOONGOZA MPAKA SASA:
PositionPlayerTeamGoals
1Sergio AgueroMan. City14
2Diego CostaChelsea12
3Alexis SanchezArsenal9
4Charlie AustinQPR8
5Papiss CisseNewcastle7
5Saido BerahinoWest Brom7
5Wilfried BonySwansea7
5Diafra SakhoWest Ham7
5Graziano PelleSouthampton7
10Leonardo UlloaLeicester6
Jonny Evans anaweza kuanza Mechi hii baada ya Mechi iliyopita kutoka Benchi kuchukua nafasi ya Chris Smalling alieumia na hiyo ikiwa Mechi yake ya kwanza baada nae kukaa nje kwa maumivu tangu Septemba.
Majeruhi wengine wa Man United waliopona na wanaweza kupata namba ni Phil Jones na Rafael lakini Angel di Maria, Luke Shaw na Daley Blind bado wako nje wakijiuguza.
Liverpool wanaweza kuwatumia Wachezaji wao waliokuwa wameumia, Adam Lallana, Kolo Toure na Mario Balotelli, ambao sasa wamepona na kurudi Mazoezini.

Ingawa Wachambuzi wengi waliiponda Man united ilipoifunga Southampton kwenye Mechi yao ya mwisho kwa kuwa na Shuti 3 tu Golini na kushinda 2-1 ukilinganisha na Southampton waliolenga mara 32, lakini huo ulikuwa ushindi wao wa 5 mfululizo kwenye Ligi na kuwarusha hadi Nafasi ya 3.

Liverpool, ambao wako Pointi 7 nyuma ya Man United, Msimu huu wamedidimia ukilinganisha na uliopita ambao waliukosa Ubingwa kidogo tu baada ya Man City kuwapiku.
Hivi sasa wako kwenye mbio za Mechi 5 bila kufungwa lakini wametoka Sare katika Mechi zao za mwisho dhidi ya Sunderland kwenye Ligi na FC Basel kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI ambayo iliwakosesha kusonga na sasa kutupwa kucheza EUROPA LIGI.
Licha ya Timu hizi mbili kuonyesha udhaifu wa aina yake Msimu huu, mtanange wa Man United na Liverpool daima ni Bigi Mechi huko England na Dunia nzima ya Soka. 
"Manchester United wameshinda Mechi 10 kati ya 12 walizocheza mwisho Uwanjani Old Trafford lakini kwenye Mechi ya mwisho Uwanjani hapo Liverpool walishinda Bao 3-0 kwa Penati 2 za Steven Gerrard, ambae pia alikosa moja, na Luis Suarez kufunga Bao la 3.
-Hii itakuwa Mechi ya 191 kati ya Mahasimu hawa huku Man united wakiongoza kwa kushinda Mechi 75, Liverpool 64 na Sare 51.
Chelsea wapo kileleni wanapointi 39 baada ya kuifunga bao 2-0 Hull City.
MSIMAMO ULIVYO MPAKA SASA"
Premier League Standings
PosTeamPLWDLGFGAGDPts
1Chelsea16123136132339
2Manchester City16113233141936
3Manchester United158432617928
4West Ham United168442719828
5Southampton1682625131226
6Arsenal167542819926
7Newcastle United166551822-423
8Swansea City156452017322
9Liverpool156361919021
10Tottenham Hotspur156361821-321
11Stoke City165471821-319
12Aston Villa165471020-1019
13Everton154652423118
14West Bromwich Albion164571520-517
15Sunderland1621041424-1016
16Crystal Palace163671924-515
17Burnley163671124-1315
18Queens Park Rangers154291627-1114
19Hull City162771523-813
20Leicester City1624101527-1210

No comments:

Post a Comment