BUKOBA SPORTS

Tuesday, December 2, 2014

MANCHESTER UNITED 2 vs 1 STOKE CITY, FELLAINI NA MATA WAIPA USHINDI UNITED!


2-1
Bao la kwanza limefungwa na M. Fellaini kipindi cha kwanza dakika ya 21, Bao la kichwa na bao la pili lilifungwa dakika ya 59 na Mata kwa frii kiki iliyonyookea moja kwa moja langoni mwa lango la Stoke City.
Wameichapa Stoke City Bao 2-1 na kubakia Nafasi ya 4 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England huku wakipata ushindi wao wa 4 mfululizo kwenye Ligi baada ya Miezi 12.

Wakicheza bila Majeruhi Nahodha wao Wayne Rooney na Angel Di Maria, Bao za Man United zilifungwa na Marouane Fellaini, Dakika ya 21, na Frikiki ya Dakika ya 59 ya Juan Mata ambayo Marcos Rojo alidai kuigusa kwa Kichwa na kutinga.

Kama Goli hilo atapewa Rojo basi hilo ni Bao lake la kwanza kwa Man United.
Bao la Stoke lilifungwa na Steven N’Zonzi Dakika ya 39.
Fellaini ndie kaifungia bao Man United kwa kichwaFellaini akifunga bao la kwanza kwa Man UnitedFellaini akishangilia bao lakeFellaini akishangilia na kupongezwa na wenzake..wa UnitedNzonzi alisawazisha bao na kufanya 1-1 kipindi cha kwanza.United hoi!!1-1Marcos Rojo aliiwezesha United kupata bao la Ushindi kwa frii kiki aliyopiga Juan MataMpira ulizama moja kwa mojaJuan Mata akishangilia.Asante Juan!Van Persie akilalamika kwa Mwamuzi baada ya kuangushwa Shangwe!!! kwa Kipa De Gea!!
Wilson kaanza leo, Rooney hakucheza katika mechi hii.

No comments:

Post a Comment