Swansea ndio walitangulia kufunga Bao kupitia Straika wa Ivory Coast Wilfried Bony na West Ham kujibu mapigo kwa Bao 2 za Vichwa za Andy Carroll na moja la Diafra Sakho, Straika kutoka Senegal.
Dakika 2 tu baada ya kupigwa Bao la Pili, Swansea walibaki Mtu 10 baada ya Kipa wao Lukasz Fabianski kupewa Kadi Nyekund kwa kumchezea Rafu Diafra Sakho lakini Refa kwanza alipeta Faulo hiyo na kumwacha Sakho aende kufunga lakini alikosa baada ya kupiga Posti na Refa Chris Foy kuamua kumtoa Kipa huyo wa zamani wa Arsenal.
No comments:
Post a Comment