BUKOBA SPORTS

Monday, December 8, 2014

SOUTHAMPTON v MAN UNITED LEO HII JUMATATU SAA 5:00 USIKU NDANI YA UWANJA WA SAINT MARY.

Man United baada ya kuichapa Stoke City Jumanne iliyopita na huo ukiwa ushindi wao wa 4 mfululizo kwenye Ligi Kuu England, Jumatatu Usiku Manchester United wanasafiri kwenda huko Uwanja wa Saint Mary kucheza na Southampton ambayo iko Nafasi ya 3 na wakishinda watatwaa wao Nafasi ya 3.

Lakini Southampton, chini ya Ronald Koeman ambae ashawahi kukorofishana na Meneja wa Man United Louis van Gaal wote walipokuwa Ajax Mwaka 2009, si Timu ya kubeza.
Hata hivyo, katika Mechi zao mbili zilizopita Southampton wamepata vichapo viwili mfululizo toka kwa Manchester City na Arsenal.

No comments:

Post a Comment