Connor Wickham alianza kuifungia bao Sunderland dakika ya 19 nao City walisawazisha bao hilo haraka kupitia kwa Sergio Agüero dakika ya 21 baada ya kulishwa mpira na Stevan Jovetic na kufanya 1-1.
Baadae dakika ya 39 Stevan Jovetic aliifungia bao la kuongoza kwa kufanya 2-1 dhidi ya Sunderland kwa Ushirikiano safi kupitia kwa Sergio Agüero na mpira kwenda mapumziko kwa bao 2-0 City wakiwa mbele.
Kipindi cha pili dakika ya 55 Pablo Zabaleta aliwafungia bao la tatu na kufanya 3-1 na kuweka mambo kuwa magumu kwa Sunderland.
Bao la nne lilifungwa tena na Sergio Agüero dakika ya 71 kipindi cha pili na kufanya 4-1 dhidi ya Sunderland.
No comments:
Post a Comment