BUKOBA SPORTS

Saturday, February 21, 2015

KOCHA WA ARSENAL ARSENE WENGER AWATUMIA SALAMU CRYSTAL PALACE, ASEMA WAJIANDAE KWA KIPIGO! ASIFU FOWADI YAKE YA SASA.

Hadi sasa Arsenal kwenye Ligi Kuu England wamefunga Mabao 47 wakiwa nyuma ya Chelsea, Bao 55, na Manchester City, Bao 51, huku Alexis Sanchez, Olivier Giroud, Santi Cazorla, Mesut Ozil na Danny Welbeck wakifunga Bao 35 kati ya hizo 47.
Wenger alieleza: “Fowadi kali ya Ligi Kuu England inapaswa kufunga kati ya Goli 70 hadi 100 kwa Msimu. Bado hatujafikia huko lakini hii ya sasa ndio bora tangu enzi za kina Thierry Henry!”
Tangu Jana Thierry Henry ametua huko Arsenal na kuwa rasmi kama mmoja wa Makocha wao.
Wenger aliongeza: “Wikiendi hii ni mara ya kwanza ambayo tunaweza kuwapanga Mafowadi wetu wote na hii itatupa nafasi ya kuona nini uwezo wao.”
Kuhusu Olivier Giroud, Wenger alifafanua: “Staili ya Giroud si ile ya kuvutia sana kama Robin van Persie lakini amezidi kuimarika na sasa ana uwezo mkubwa!”
Wikiendi hii Arsenal wako Ugenini huko Selhurst Park kucheza na Crystal Palace na wanaweza kumtumia tena Kiungo wao Jack Wilshere ambae alikuwa Majeruhi kwa muda mrefu.
Kocha wa Arsenal, Arsene  WengerSanti Cazorla

No comments:

Post a Comment