BUKOBA SPORTS

Sunday, April 26, 2015

BAYERN MUNICH SASA MABINGWA BAADA YA KUICHAPA BAO 1-0 HERTHA BERLIN, SCHWEAINSTEIGER SHUJAA!


Bastian Schweinsteiger ndie aliyeifungia bao Bayern Munich walipoichapa Hertha Berlin 1-0 huko Allianz Arena jana jumamosi.

Schweinsteiger akiwaongoza wenzake kushangilia baada ya kuifunga bao 1-0 Hertha na kuiwezesha Bayern kukwapua Ubingwa kwa mara nyingine.

Mitchell Weiser katikati akikokota mpira na kumtengea Schweinsteiger

Dante akijichukulia mpira karib na kichwa cha Nico Schulz wa Hertha kwenye Uwanja wa Allianz Arena

Schweinsteiger akiwapa dole mashabiki wao

Pep Guardiola ameiongoza Bayern kushinda Kombe hili na bado ana nafasi ya kupigana mpaka mwisho Kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya mwezi ujao Mei

Schulz akijijutia baada ya kukosa nafasi ya wazi kuifunga Bayern Munich

Thomas Mueller akichuana na Valentin Stocker

Guardiola akitoa pongezi kwa Vijana wake

Bayern wana pointi 15 juu dhidi ya Timu ya pili kitu ambacho kinawafanya wanyakue Kombe hilo kwa mara ya 25.

No comments:

Post a Comment