BUKOBA SPORTS

Saturday, April 4, 2015

BUNDESLIGA: BORUSSIA DORTMUND 0 vs 1 BAYERN MUNICH, LEWANDOWSKI AIPA USHINDI BAYERN


Robert Lewandowski  akiifungia bao  Bayern Munich usiku huu dhidi ya Dortmund mpira uliomalizika kwa bao 1-0.

Wachezaji wa  Bayern Munich wakishangilia Ushindi wa wa bao 1-0 usiku huu dhidi ya Dortmund

Robert Lewandowski Dakika ya 36 Kipindi cha kwanza aliifungia bao Bayern Munich.Mechi ya Bundesliga ambayo ina Jina la Ubatizo 'DER KLASSIKER' na kipigo hiki kikidhihirisha Msimu mbovu wa Borussia Dortmund wakibaki katikati ya Msimamo wa Ligi na Bayern kuelekea kutetea Taji lao.
Bao la ushindi la Bayern lilifungwa na Mchezaji wa zamani wa Dortmund Robert Lewandowski katika Dakika ya 36.
Ushindi huu umewapa Bayern uongozi wa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Wolfsburg na Dortmund kubaki Nafasi ya 10.

Lewandowski hakushangilia baada ya kuipiga Timu yake ya Zamani Borussia Dortmund

 Pep Guardiola  akiongoza Benchi lake kushangilia..

Mfungaji wa Bao la pekee Lewandowski akichuana na Mchezaji wa  Dortmund Kevin Kampl


Timu zikijipanga kabla ya Mtanange kuanza

No comments:

Post a Comment