BUKOBA SPORTS

Saturday, April 4, 2015

YANGA YAFUNGWA 1-0 ZIMBABWE, YAFUZU KWA 5-2 KOMBE LA SHIRIKISHO, SASA KUIVAA BENFICA AU SAHEL!

Yanga imefanikiwa kuchanja mbuga katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa jumla ya mabao 5-2 ikiwa ugenini nchini Zimbabwe. Yanga wamefuzu licha ya kufungwa kwa bao 1-0 dhidi ya FC Platnum katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mandava ulio takribani Kilomita 200 kutoka mji wa Bulawayo. Mechi hiyo kali na ya kuvutia, wenyeji walipania kufunga mabao manne ili wafuzu lakini ilishindikana. Kocha Hans van der Pluijm alilazimika kumtoa mapema kinda Said Juma ‘Makapu’ kutokana na kuonekana kuzidiwa na nafasi yake kumuingiza Kelvin Yondani.

No comments:

Post a Comment