BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 29, 2015

INTERNATIONAL CHAMPIONS CUP: MAN UNITED USO KWA USO NA BARCELONA, PSG, SAN JOSE EARTHQUAKES NA CLUB AMERICA KWENYE ZIARA YA KUJPIMA NA MSIMU MPYA 2015/16

RATIBA KAMILI
Manchester United vs Club America, 17 July
Manchester United vs San Jose Earthquakes, 21 July
Manchester United vs Barcelona, 25 July
Manchester United vs PSG, 29 July

Manchester United wataivaa Barcelona ikiwa ni moja ya Mechi zao 4 huko Marekani kwenye Ziara yao ya kabla Msimu mpya wa 2015/16 kuanza.
Man United, Mabingwa wa England mara 20,watacheza na Barca ndani ya Levi's Stadium Mjini Santa Clara, California, hapo Julai 25.
Mechi hizi ni za Mashindano ya International Champions Cup ambayo Mwaka Jana, wakiwa chini ya Kocha mpya Louis van Gaal, Man United iliitwanga Liverpool 3-1 kwenye Fainali na kubeba Kombe.
Kwenye Fainali hiyo, Liverpool walitangulia kwa Penati ya Steven Gerrard lakini Man United wakajibu kwa Bao 3 za Wayne Rooney, Juan Mata na Jesse Lingard.
Kwa kuelekea Fainali, Man United walizibwaga Klabu za Italy, AS Roma na Inter Milan, na kisha kuitwanga Real Madrid.
Mechi nyingine za Man United ni huko Chicago hapo Julai 29 dhidi ya Paris St Germain na kisha dhidi ya Klabu ya Mexico, Club America, watakayocheza Mjini Seattle na ile ya Klabu ya Marekani, San Jose Earthquakes, watakayocheza kwenye Uwanja utakaotangazwa baadae.Mashindano hayo ya ICC yanatarajiwa kuanza Julai 11 na kumalizika Agosti 5 kabla tu ya Misimu mipya ya 2015/16 kuanza huko Ulaya.
Mwaka Jana kwenye Mashindano haya, Mechi kati ya Man United na Real Madrid, ambayo Man United walishinda 3-1, iliweka Rekodi huko Michigan, USA kwa kuhudhuriwa na Washabiki wengi mno ambapo Watu zaidi ya 109,000 walisheheni Uwanjani.
Mwaka Jana, chini ya Kocha mpya Louis van Gaal, Man United iliitwanga Liverpool 3-1 kwenye Fainali na kubeba Kombe.
Kwenye Fainali hiyo, Liverpool walitangulia kwa Penati ya Steven Gerrard lakini Man United wakajibu kwa Bao 3 za Wayne Rooney, Juan Mata na Jesse Lingard.
Kwa kuelekea Fainali, Man
United walizibwaga Klabu za Italy, AS Roma na Inter Milan, na kisha kuitwanga Real Madrid.

TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea
Manchester United
Barcelona
Club America
Fiorentina
LA Galaxy
New York Red Bulls
Paris Saint-Germain
Porto
San Jose Earthquakes

No comments:

Post a Comment