BUKOBA SPORTS

Sunday, April 5, 2015

JUVENTUS YAELEKEA PATAMU!! UBINGWA WANUKIA, TEVEZ ACHEKELEA!!

Mabingwa wa Italy na Vinara wa Serie A, Juventus, Jana waliichapa Empoli Bao 2-0 na kuendelea kupaa kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 14 mbele.
Magoli ya Juve yalifungwa na Carlos Tevez Dakika ya 43 na Roberto Pereyra Dakika ya 90.
Juve wameendelea kukaribia kutetea vyema Taji lao na sasa, huku Timu zote zikiwa zimecheza Mechi 39, wana Pointi 70 wakifuatiwa na AS Roma wenye 56 kisha Lazio 56 na Fiorentina 49.
Kila Timu imebakisha Mechi 9.


Kati Wiki Juve watacheza Nusu Fainali ya Coppa Italia dhidi ya Fiorentina na ndio maana Jana iliwakosa Wachezaji kadhaa ingawa wengine walikuwa na maumivu na hao ni Claudio Marchisio, Andrea Pirlo, Paul Pogba, Kwadwo Asamoah, Martin Caceres, Kingsley Coman na Romulo.

VIKOSI:
Juventus:
Buffon; Barzagli, Bonucci, Ogbonna; Lichtsteiner, Sturaro (Pereyra 77), Padoin, Vidal (Pepe 86), Evra; Tevez, Llorente (Morata 67)
Empoli: Sepe; Hysaj, Rugani, Barba, Mario Rui; Vecino, Valdifiori, Croce (Zielinski 74); Saponara; Maccarone (Mchedlidze 72), Pucciarelli (Verdi 77)
Refa: Giacomelli

No comments:

Post a Comment