BUKOBA SPORTS

Sunday, April 5, 2015

REAL MADRID 9 vs 1 GRANADA, CRISTIANO RONALDO APIGA HAT-TRICK NA KUMFUNIKA LIONEL MESSI! AKIFUNGA BAO TANO, BERNABEU PATAKATA LEO!

Granada, ambao hawajawahi kushinda Uwanjani Santiago Bernabeu tangu Januari 1974 waliposhinda 1-0 na tangu wakati huo wamecheza Mechi 20, Leo tena wameendeleza uteja kwa kubamizwa Bao 9-1 kwenye Mechi ya La Liga na Real Madrid huku Cristiano Ronaldo akipiga Bao 5.
Hadi Mapumziko Real walikuwa mbele kwa Bao za Garreth Bale na Hetitriki ya Ronaldo.
Kipindi cha Pili Karim Benzema alifunga Bao 2, Ronaldo kuongeza 2 na Bao moja Granada kujifunga wenyewe kupitia Mainz.
Bao pekee la Granada lilifungwa na Robert Ibanez.
Ushindi huu, ambao ni mkubwa kwa Real tangu 1967, umeifanya Real, walio Nafasi ya PIli kwenye La Liga, wawakaribie Vinara Barcelona wakiwa Pointi 1 nyuma yao.
Pia kwenye vita ya Pichichi, Tuzo ya Mfungaji Bora wa La Liga, Ronaldo ambae alikuwa nyuma ya Lionel Messi kwa Bao moja, sasa yuko mbele kwa Bao 4 akiwa na Jumla ya Mabao 36.

Ronaldo akishangilia
Dakika ya 38 Ronaldo alifunga Hat-trick bao la tatu kwake na kufanya 4-0 dhidi ya Granada na ndani ya dakika 8 na Mtanange kwenda mapumziko kwa bao hizo 4-0 dhidi ya Granada kwenye Uwanja wa Nyumbani wa  Bernabeu.
Cristiano Ronaldo Aalifunga tena bao la tatu kwa shuti kali na kufanya 3-0 dhidi ya Granada katika dakika ya 36
Cristiano Ronaldo aliwapachikia bao la pili Real baada ya kusogezewa pasi tamu na kufunga bao la pili na kufanya 2-0 katika dakika ya 30.
Bao la kwanza lilifungwa na Gareth Bale dakika ya 25 baada ya kuwachambua mabeki wa Granada na pamoja na kipa wao na kufunga bao la kwanza kwa Real Madrid kwa kufanya 1-0 dhidi ya Granada.Gareth Bale akimkacha kipa wa GranadaRonaldo akiwavizia vizia Granada mchana huu..kuona kama aitaipandisha Real Juu karibu na Barca.
James Rodriguez Arudi
VIKOSI:
Real Madrid: Casillas; Arbeloa, Ramos, Varane, Marcelo; Modric, Kroos; Bale, Rodriguez, Ronaldo; Benzema.
Granada: Olazabal; Foulquier, Babin, Mainz, Carlos; Rico, Iturra; Ibanez, Rochina, Candeias; El Arabi.


James Rodriguez akipasha na Kwenye mtanange huu akitegemewa kuonesha kiwango safi baada ya kukosa mechi kadhaa.

No comments:

Post a Comment