BUKOBA SPORTS

Sunday, April 26, 2015

FULL TIME: ARSENAL 0 vs 0 CHELSEA, JOSE MOURINHO BADO AZIDI KUMWANGAISHA NJE NDANI ARSENE WENGER!! LEO WAMALIZANA KWA SARE!

Jose Mourinho sasa amefikisha Mechi 13 bila kufungwa na Arsene Wenger baada ya Leo Arsenal na Chelsea kutoka Sare ya 0-0 Uwanjani Emirates na sasa Chelsea wanahitaji Pointi 6 kati ya Mechi zao 5 zilizobaki kutwaa Ubingwa.
Chelsea, chini ya Mourinho, imeichapa Arsenal ya Wenger mara 7 na kutoka Sare 6 na Leo Mourinho alihakikisha kuwa Rekodi yake haichafuliwa kwa kucheza kwa tahadhari kubwa ya kujilinda na kuwaacha Arsenal watawale Mpira. Sare hii imeibakisha Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Chelsea na wamefungana kwa Pointi na Man City waliokamata Nafasi ya Pili kwa Ubora wa Magoli lakini Arsenal wamecheza Mechi 1 pungufu.
Man United ipo Nafasi ya 4 ikiwa Pointi 2 nyuma ya Arsenal na City.
Kocha Jose Mourinho wa Chelsea
Patashika kwenye lango la Chelsea

No comments:

Post a Comment