BUKOBA SPORTS

Saturday, May 2, 2015

LEO USIKU NI PATASHIKA NCHINI TUNISIA... SOUSSE, NI ETOILE DU SAHEL vs YANGA SC.

MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, Leo hii wako Stade Olympique Sousse Mjini Sousse Nchini Tunisia kurudiana na Etoile Du Sahel kwenye Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Yanga na Etoile Du Sahel zilitoka Bao 1-1 na Bao hizo zilifungwa na Kepteni wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' kwa Penati na Etoile kusawazisha kwa Bao la Mohamed Amine Ben Amor.
Mechi hii ya Leo itaanza Saa 3 Usiku, kwa Saa za Bongo, na ili kusonga mbele Yanga wanahitaji ushindi au Sare ya Bao nyingi kuanzia 2-2.
Wakati Kocha wa Yanga kutoka Holland, Hans van der Pluijm, akisisitiza wana kazi ngumu na wanahitaji kupigana, Kocha wa Etoile du Sahel, Faouzi Benzarti, ametamba kazi yao ni nyepesi.


Kikosi cha Yanga kilichokwenda Tunisia ni:
Makipa: Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’
Mabeki : Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Edward Charles, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ’Juma Abdul, Rajab Zahir, Mbuyu Twite na Kevin Yondan.
Viungo: Nizar Khalfan, Andrey Coutinho, Salum Telela na Said Juma ‘Makapu’
Mastraika: Hussein Javu, Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Mrisho Ngasa, Jerry Tegete na Simon Msuva.
 

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:
RATIBA/MATOKEO
Ijumaa Mei 1

Etancheite -Congo DR 0 vs Wari Wolves - Nigeria 1 [1-3]
Club Africain - Tunisia 1 vs Association Sportive Olympique de Chlef - Algeria 0 [2-1]
Jumamosi Mei 2
2100 E.S. Sahel v Yanga

Mechi nyingine:
ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast v Onze Createurs - Mali [1-0]
Hearts of Oak - Ghana vs  Djoliba AC - Mali [2-1]
Orlando Pirates - South Africa vs CF Mounana - Gabon [2-2]
Fath Union Sport de Rabat - Morocco vs Al Zamalek - Egypt [0-0]
AS Vita Club Congo DR vs Royal Leopards - Swaziland [0-1]

No comments:

Post a Comment