BUKOBA SPORTS

Sunday, May 3, 2015

FULL TIME: CHELSEA 1 vs 0 CRYSTAL PALACE, BLUES SASA MABINGWA ENGLAND MSIMU HUU 2014/15


Chelsea leo jumapili wametwaa Ubingwa wao wa 4 wa Ligi Kuu England baada ya kuifunga Crystal Palace Bao 1-0 Uwanjani Stamford Bridge.Huu ni Ubingwa wao wa kwanza tangu 2010 na umekuja huku wakiwa na Mechi 3 mkononi baada ya kufikisha Pointi 83 ambazo haziwezi kufikiwa na Timu nyingine.Hadi Mapumziko Chelsea walikuwa mbele kwa Bao la Dakika ya 45 alilofunga Eden Hazard baada ya Penati yake kuokolewa na Kipa Speroni na kumrudia yeye na kumalizia kwa Kichwa.
Penati hiyo ilitolewa na Refa baada ya Hazard kuangushwa na James McArthur ndani ya Boksi.

Eden Hazard dakika ya 45 mwishoni mwa kipindi cha kwanza na kufanya 1-0 dhidi ya Crystal Palace.
VIKOSI:
Chelsea:
Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Fabregas, Matic, Ramires, Willian, Hazard, Drogba.
Akiba: Cech, Luis, Zouma, Mikel, Remy, Cuadrado, Loftus-Cheek.

Crystal Palace: Speroni, Mariappa, Delaney, Dann, Ward, McArthur, Ledley, Mutch, Puncheon, Bolasie, Zaha.
Akiba: Hangeland, Sanogo, Hennessey, Jedinak, Murray, Lee, Kelly.
Refa: Kevin Friend

No comments:

Post a Comment