BUKOBA SPORTS

Sunday, May 3, 2015

FULL TIME: SIMBA SC 2 vs 1 AZAM FC


Kikosi cha Azam FC kilichoanza leo. (Picha na Francis Dande)

Kikosi cha Simba.

Waamuzi wa mchezo wa Simba na Azam wakiwa katika picha ya pamoja na manahodha wa timu zote kabla ya mchezo.
Simba imewachapa Mabingwa wa zamani Azam FC Bao 2-1 na kujiletea matumaini makubwa ya kufuzu Nafasi ya Pili na hivyo kucheza Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho Mwakani.
Simba wapo Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 tu nyuma ya Azam FC walio Nafasi ya Pili nyuma ya Yanga ambao tayari wameshatwaa Ubingwa.
Ikiwa Jumatano Yanga wataifunga Azam FC au kutoka Sare, Simba wanaweza kuipiku Azam FC katika Mechi za mwisho za Ligi zitakazochezwa Jumamosi Mei 9.


Beki wa Azam FC, Shomari Kapombe akichuana na mshambuliaji wa Simba, Said Ndemla.

Himid Mao akijaribu kumzuia Said Ndemla wa Simba.
Katika Mechi ya Leo, Simba walinufaika kwa kucheza na Mtu 10 Azam FC baada Kiungo wao Abubakar Salum kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 38.
Simba walitangulia kufunga kwa Bao la Ibrahim Ajibu, Dakika ya 47, na Mudathir Yahya kuisawazishia Azam FC Dakika ya 57 lakini Ramadhan Singano akapiga Bao la Pili na la ushindi kwa Simba katika Dakika ya 74.
Huko Tanga, Coastal Union imeitandika Stand United Bao 3-1 na huko Manungu, Morogoro, Mtibwa Sugar imeichapa Ruvu Shooting 2-0.


mshambuliaji wa Simba, Said Ndemla akimtoka Himid Mao.

Emmanuel Okwi akichuana na beki wa Azam FC, Agrey Moris.

Agrey Moris na akichuana na Emmanuel Okwi.

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.

Beki wa Azam FC, Agrey Moris akimiliki mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Singano 'Messi" akishangilia kwa staili ya aina yake baada ya kuipatia timu yake bao la pili.
Raha ya ushindi.


Mashabiki wa Simba wakishuhudia pambano hilo.

No comments:

Post a Comment