BUKOBA SPORTS

Monday, May 4, 2015

FULL TIME: HULL CITY 1 vs 3 ARSENAL, GUNNERS WAJICHOMEKA NDANI YA "TOP 4" NAFASI YA UHAKIKA KUCHEZA UEFA MSIMU UJAO, RAMSEY AKIFUNGA BAO NA ALEXIS SANCHEZ AKITUPIA BAO MBILI USIKU HUU!

Mtanange umemalizika bao 3-1 kwenye Uwanja wa  KC Stadium  leo Jumatatu kwenye kipute cha kipekee kumalizia mzunguko uliokuwa umeanza jumamosi na Arsenal kuibuka kidedea kwa bao 3-1.

Sanchez

Ndani ya Uwanja  KC Stadium furaha kwa kijana
Sanchez akimpelekesha kipa  Steve Harper kwa kumzunguka
Aaron Ramsey akiachia shuti kali
Kipa Steve Harper akiwa hoi baada ya kufungwa bao jingine na kubaki akiduwaa!
Kipindi cha pili dakika ya 56 Stephen Quinn aliwafanikishia bao na kufanya 3-1 baada ya kupewa pasi na Ahmed El Mohamady na kufunga bao hilo kwa kichwa. Mpaka dakika 90 zinamalizika Arsenal 3-1 Hull City. Ushindi huu unawaweka pazuri kwenye nafasi ya nne bora Arsenal kwa kufikisha pointi 70 wakiwa nafasi ya 3  na kulingana na City ambao wako nafasi ya pili wenye nao pointi 70 wakitofautiana magoli ya kufunga. Hull wako nafasi ya 17 wakiwa chupuchupu kwenye msitari wa kushuka daraja wakiwa na pointi zao 34. Nafasi ya nne wako Man United ambao wako nyuma kwa pointi 5 wenye pointi 65.Alexis Sánchez dakika ya 45 kipindi cha kwanza aliwafungia bao la tatu Arsenal na kufanya 3-0 likiwa bao lake la pili kwa mtanange huu na mpira kwenda mapumziko wakiongoza Gunners wakiwa mbele ya bao 3-0 kwenye Uwanja wa Ugenini KC Stadium.Alexis akishangilia bao lake
Alexis Sánchez dakika ya 28 kipindi cha kwanza na bao la pili lilifungwa dakika 33 na Aaron Ramsey baada ya Santi Cazorla kutoa usaidiaji wa bao hilo kupatikana.Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger  Kashuhudia Vijana wake Uwanjani KC Stadium  wakimenyana na Timu ya Hull ambayo ipo nafasi ya 17 Kwenye Ligi kuu England Msimu huu unaelekea Ukingoni kumalizika.
VIKOSI:
Hull XI:
Harper, Chester, Huddlestone, Brady, Livermore, McShane, Dawson, Aluko, Elmohamady, N'Doye, Quinn

Akiba: McGregor, Rosenior, Bruce, Meyler, Hernandez, Jelavic, Robertson
Arsenal XI: Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Ramsey, Ozil, Alexis, Giroud
Akiba: Sczcesny, Gabriel, Rosicky, Gibbs, Wilshere, Walcott, Flamini

No comments:

Post a Comment