BUKOBA SPORTS

Tuesday, May 5, 2015

MAJOGOO LIVERPOOL KUWAWEKEA GWARIDE LA HESHIMA MABINGWA CHELSEA JUMAPILI!

Liverpool Jumapili ijayo Uwanjani Stamford Bridge watawajibika kujipanga Mistari miwili kuwakaribisha Mabingwa Wapya wa England, Chelsea, wakati wakiingia Uwanjani kabla ya Mechi yao ya Ligi Kuu England.
Gwaride hilo la heshima ni utamaduni wa huko England wa kuwaheshimu Mabingwa wapya na Mwaka 2007 Chelsea waliwahi kuwaheshimu Manchester United mara tu baada ya kutwaa Ubingwa na Mechi iliyofuata ya Man United kuchezwa Stamford Bridge na Wachezaji wa Chelsea kuweka Gwaride la Heshima.
Jana Jumapili Chelsea walitwaa Ubingwa wa England baada ya kuwachapa Crystal Palace Bao 1-0 ukiwa ni Ubingwa wao wa kwanza tangu 2010 na wa 4 tangu Mrusi Roman Abramovich aanze kuimiliki.
Lakini hili la Kikosi cha Steven Gerrard kuwapigia Makofi Mabingwa wapya Chelsea wakiingia Uwanjani bila shaka litawafurahisha Mashabiki wa Chelsea ingawa Meneja wa Klabu hiyo Jose Mourinho ameuponda utaratibu huo.

Mourinho amesema: "Sipendi hili. Nadhani Spain tuliwahi kufanyiwa mara moja nlipokuwa Real Madrid. Lakini kama ni utamaduni sawa!"
Lakini Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, ambae aliwahi kufanya kazi Chelsea chini ya Mourinho, amesema Chelsea inahitaji heshima.
Alipoulizwa kama Chelsea wanastahili Gwaride la Heshima kutoka Liverpool, Rodgers alijibu: "Wanastahili. Klabu yetu ina misingi ya utu na heshima. Yeyote anaekuwa Bingwa wanamfanyia hilo!"
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumatatu Mei 4

22:00 Hull vs Arsenal
Jumamosi Mei 9
14:45 Everton vs Sunderland
17:00 Aston Villa vs West Ham
17:00 Hull vs Burnley
17:00 Leicester vs Southampton
17:00 Newcastle vs West Brom
17:00 Stoke vs Tottenham
19:30 Crystal Palace vs Man United
Jumapili Mei 10
15:30 Man City vs QPR
18:00 Chelsea vs Liverpool
Jumatatu Mei 11
22:00 Arsenal vs Swansea

No comments:

Post a Comment