BUKOBA SPORTS

Monday, May 4, 2015

RATIBA YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE, NUSU FAINALI: JUMANNE NI PATASHIKA! JUVENTUS vs REAL MADRID, JUMATANO NI MAGWIJI BARCELONA vs BAYERN MUNICH!

Yale Mashindano makubwa kabisa kwa Klabu Barani Ulaya, UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, Jumanne yataanza kuchezwa Mechi zake za kwanza za Nusu Fainali.
Jumanne Usiku, Uwanja wa Juventus Arena Jijini Turin Nchini Italy, utakuwa ni dimba la Mechi ya Nusu Fainali ya kwanza ya UEFA CHAMPIONS LIGI, kati ya Juventus na Mabingwa Watetezi wa Mashindano haya, Real Madrid.
Nusu Fainali nyingine ya UCL ni Jumatano huko Nou Camp Mjini Barcelona Nchini Spain, ambapo Wenyeji Barcelona wanaoongoza La Liga, watawakaribisha Mabingwa wa Germany Bayern Munich ambayo sasa ipo chini ya Kocha Pep Guardiola ambae alijizolea sifa kubwa kwa kutwaa Mataji kibao akiwa na Barcelona kabla kung'atuka Miaka michache iliyopita.
www.bukobasports.comMarudiano ya Nusu Fainali hizi za UCL yatafanyika Wiki ijayo Jumanne na Jumatano, Mei 12 na 13.
UEFA CHAMPIONS LIGI
Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Nusu Fainali-Mechi za Kwanza
Jumanne Mei 5
Juventus FC vs Real Madrid CF
(Refa: Martin Atkinson)
Jumatano Mei 6
FC Barcelona vs Bayern Munich

Mechi za Marudiano
Jumanne Mei 12
Bayern Munich vs FC Barcelona
Jumatano Mei 13
Real Madrid CF vs Juventus FC

No comments:

Post a Comment