BUKOBA SPORTS

Monday, May 4, 2015

ULUGURU U-20 SUPER CUP 2015 MEI 18


MICHUANO ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya ‘Uluguru U-20 Super Cup 2015’ inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 18, mwaka huu, kwenye viwanja vya Jamhuri na Tumbaku, mkoani Morogoro.
Ofisa habari wa mashindano hayo, Adam Kassim alisema michuano hiyo itashirikisha timu za vijana (U-20) za timu za ligi kuu Bara, daraja la kwanza na zile za vituo vya kukuza soka la vijana (akademi).
Kassim alisema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vya wanasoka chipukizi nchini na kutoa nafasi kwa timu mbalimbali zikiwemo za ligi kuu kuangalia vipaji kupitia michuano hiyo.


KIKOSI cha Azam FC (U-20) nacho kimealikwa kushiriki michuano hiyo ya vijana ya Uluguru Super Cup 2015.
Alisema michuano hiyo itashirikisha timu kumi na sita zitakazogawanywa katika makundi manne na timu mbili za juu kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya robo fainali.
Ofisa habari huyo alisema mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh.Mil 1.2/=, wa pili atapata Sh.600,000/=, wa tatu atapata Sh.300,000/=, timu yenye nidhamu bora itapata Sh.100,000/= na mfungaji bora ataibuka na Sh.50,000/=.
Kassim alisema fomu kwa timu shiriki zimeshaanza kutolewa na mwisho kwa timu zinazotaka kushiriki kuthibitisha ushiriki wao ni Mei 12.
“Maandalizi yapo vizuri na milango ipo wazi kwa timu yoyote ya ligi kuu, daraja la kwanza na zile za Akademi zilizo tayari kushiriki na tunaweza kuwasiliana kwa namba 0714 743276”, alisema.

No comments:

Post a Comment