BUKOBA SPORTS

Saturday, May 2, 2015

SERIE A: RATIBA WIKIENDI HII!! VINARA JUVE WANAHITAJI POINTI MOJA TU KUWA BINGWA KWA MARA YA 4 MFULULIZO!! LEO WANA UC SAMPDORIA SAA 1.

Juventus wanahitaji Pointi 1 tu wakicheza Ugenini hii leo na Sampdoria ili watae Ubingwa wa Ligi ya Italy Serie A kwa mara ya 4 mfululizo.
Sampdoria hivi sasa inasuasua na hawajashinda katika Mechi zao 5 zilizopita huku Kocha wao Sinisa Mihajlovic akiwa mguu nje mguu ndani.

Jumatano iliyopita Juve waliichapa Fiorentina Bao 3-2 lakini katika Mechi zao 2 zilizopita za Ugenini wamefungwa na kufikisha vipigo kwenye Serie A kuwa Mechi 3 kwa Msimu mzimu.
Lakni Kocha wao, Massimiliano Allegri, amepuuza hilo na kudai kwa kuwa wako Pointi 14 mbele kufifia kwa kutilia mkazo Mechi ndio sababu.
Juve wana Pointi 76 kwa Mechi 33 na wamebakisha Mechi 5 wakifuatiwa na Lazio wenye Pointi 62 kwa Mechi 33.

SERIE A: RATIBA
Jumamosi Mei 2
19:00 UC Sampdoria vs Juventus FC
21:45 US Sassuolo Calcio vs U.S. Citta di Palermo
Jumapili Mei 3
13:30 AS Roma vs Genoa CFC
16:00 Atalanta vs SS Lazio
16:00 Inter Milan vs AC Chievo Verona
16:00 Hellas Verona FC vs Udinese Calcio
16:00 ACF Fiorentina vs AC Cesena
21:45 SSC Napoli vs AC Milan
Jumatatu Mei 4
21:45 Cagliari Calcio vs Parma FC
Jumanne Mei 5
16:00 Torino FC vs Empoli

No comments:

Post a Comment