Mmoja wa waliodai hivyo ni Piers Morgan ambae ni Mwandishi na Mwendesha Kipindi cha TV ambae alikasirishwa na Jana kutandikwa 3-2 na Olympiakos ya Ugiriki katika Mechi ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS.
Hiki ni kipigo cha pili kwa Arsenal katika Kundi lao baada ya kuchapwa 2-1 na Dinamo Zagreb huko Croatia.
Piers Morgan alisema: “Ulikuwa ni uchezaji mbovu katika Mechi za Ulaya ambao sijapata kuuona katika muda wake wote Wenger akiwa Arsenal.”
Aliongeza: “Tulicheza ovyo dhidi ya Timu iliyofungwa mara zote 12 ikicheza England na kufungwa Mabao 37-3. Lakini Jana wametubamiza!” Morgan alilalamika: “Wenger Siku zote ana visingizio, mara Uwanja, mara Fedha, Bodi, Hali ya Hewa. Kila kitu ni visingizio lakini si yeye Wenger. Jana visingizio vimeisha. Ni yeye!”
Morgan amedai Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp, ndio anafaa kumbadili Wenger.
Mechi zinazofuata kwa Arsenal kwenye Kundi F la UCL ni Mechi mbili mfululizo dhidi ya Bayern Munich ambao wameshinda Mechi zao zote 2 kwa kuzibamiza 3-0 Olympiakos huko Ugiriki na 5-0 Dinamo Zagreb huko Munich.
Labda Wenger sasa ameifikisha Arsenal mahala ambapo inabidi ampe kijiti mwalimu mwingine, kufeli kushindwa kubeba taji lolote kubwa tangu kikosi chake kilipotwaa EPL bila kufungwa msimu wa 2003/04, Arsenal imekwama. Makombe mawili ya FA Cup bado hayakidhi haja bila uwepo wa taji la EPL au lolote la ulaya.
No comments:
Post a Comment