BUKOBA SPORTS

Thursday, October 1, 2015

CRISTIANO RONALDO AFIKISHA MAGOLI 501 KATIKA MAISHA YAKE YA SOKA!

BAO 2 za Cristiano Ronaldo hapo Jana wakati Real Madrid inaichapa Malmo 2-0 kwenye Mechi ya Kundi A la UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, zimemfanya afikishe Jumla ya Magoli 501 katika maisha yake ya Soka.
Ronaldo amecheza Jumla ya Mechi 753 kwa Real, Man United, Sporting Lisbon na Nchi yake Portugal. Miongoni mwa hizo Bao 501 ni Mabao 323 aliyoifungia Real katika Mechi 308 na kumfanya afungane na Mfungaji Bora katika Historia ya Real, Raul, ambae alichukua Mechi 400 zaidi ya Ronaldo kufikia idadi hiyo.
RONALDO- Rekodi:
-Hetitriku 37
-UCL: Mfungaji Bora Bao 82 (5 zaidi ya Lionell Messi)
-Portugal: Bao 55 Mechi 122
-Penati: Bao 81
-Frikiki: Bao 45
-Man United: Bao 118
-Sporting Lisbon: Bao 5

No comments:

Post a Comment