Dakika 5 baada ya Mertesacker kutolewa nje, Diego Costa alifunga Bao pekee na la ushindi kwa Chelsea.
Wenger ameeleza: “Costa amesababisha Wachezaji wetu Wawili wapewe Kadi Nyekundu katika Mechi zetu 2 zilizopita. Je ni uamuzi sahihi au hapana? Sijui. Huo ni ukweli bila kumtuhumu chochote!”
Msimu huu, Arsenal wamezoa Kadi Nyekundu 3 na zote ni za kwenye Mechi dhidi ya Chelsea baada ya pia Santi Cazorla kutolewa nje katika Mechi hiyo hiyo aliyotolewa Gabriel huko Stamford Bridge.
Arsenal wamezoa Kadi Nyekundu 7 kwenye Mechi na Chelsea na hizo ni nyingi kupitana kwenye mapambano yao na Timu nyingine yeyote kwenye Ligi Kuu England.
Wenger amesema: “Refa alikuwa mwepesi kutoa Kadi Nyekundu. Lakini tulilikabili tukio hilo vizuri na tulistahili Sare.”
Alipohojiwa kama Costa alitengeneza tukio hilo, Wenger alijibu: “Ndio. Hiyo ndio Gemu ya Straika. Diego Costa ni mzuri kwa hayo!”
Lakini Bosi wa Chelsea, Guus Hiddink, hakukubaliana na amesema: "Kulikuwa hamna wasiwasi. Ni pasi safi na Costa angeweza kwenda moja kwa moja kumkabili Kipa Petr Cech lakini aliangushwa. Hilo ni wazi!”
No comments:
Post a Comment