BUKOBA SPORTS

Monday, January 25, 2016

CHAN 2016: CAMEROUN 3-1 CONGO DR, ETHIOPIA 1 v 2 ANGOLA. (CAMEROUN NA CONGO DR) WAUNGANA ROBO FAINALI

Kundi B la Fainali za 2016 African Nations Championship (Chan 2016), ambazo ni Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wachezao ndani ya Afrika, ambazo zinachezwa huko Rwanda, Leo zimemaliza Mechi zao Cameroun kuungana na Congo DR ambao walikwishafuzu kabla ya leo.
Congo DR, ambao walikuwa tayari wamefuzu kabla Mechi hii, Leo walifungwa 3-1 na Cameroun ambayo sasa imeungana nao kucheza Robo Fainali.
Bao za Cameroun zilifungwa na Cameroon Yazid Atouba, Dakika ya 40, Moumi Ngemaleu, 52 na Samuel Nlend, 64 wakati Bao la Congo DR lilifungwa Dakika ya 47 Jean-Marc Makusu.
Katika Mechi nyingine ya Kundi B, Angola iliichapa Ethiopia 2-1 lakini zote ziliaga Mashindano kwa kumaliza Nafasi za 3 na 4 katika Kundi B.

Ary Papel ndie aliwapa Angola Bao zao 2 katika Dakika za 54 na 73 na lile la Ethiopia kufungwa Dakika ya 75 na Seyum Tesifaye.
Jumanne zipo Mechi 2 za mwisho za Kundi C ambalo bado hakuna iliyofuzu mapema ingawa Nigeria wana nafasi kubwa.

Kundi B la Fainali za 2016 African Nations Championship (Chan 2016), ambazo ni Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wachezao ndani ya Afrika, ambazo zinachezwa huko Rwanda, Leo zimemaliza Mechi zao Cameroun kuungana na Congo DR ambao walikwishafuzu kabla ya leo. RATIBA/MATOKEO
Jumatatu Januari 25

Ethiopia 1 v Angola 2
Cameroon 3 v DR Congo 1

Jumanne Januari 26
Guinea v Nigeria Rubavu 16:00
Niger v Tunisia Stade Régional de Nyamirambo 16:00
 

Jumatano Januari 27
Zambia v Mali Stade Régional de Nyamirambo 16:00
Uganda v Zimbabwe Amahoro, Kigali 16:00

ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 30

Rwanda v Congo DR
Cameroun v Ivory Coast

Jumapili Januari 31
Mshindi Kundi D v Mshindi wa 2 Kundi C
Mshindi Kundi C v Mshindi wa 2 Kundi D

NUSU FAINALI
Jumatano Februari 3

Rwanda/Congo DR v Mshindi Kundi D/Mshindi wa 2 Kundi C

Alhamisi Februari 4
Mshindi Kundi C/Mshindi wa 2 Kundi D v Cameroun/Ivory Coast

Jumapili Februari 7
Mshindi wa 3
FAINALI

No comments:

Post a Comment