Juan Mata kaifungia bao la tatu Man United dakika ya 83 baada ya kupata pasi safi kutoka Anthony Martial na kufanya Man United waongoze bao 3-1.
Blind dakika ya 65 aliwapachikia bao la pili Man United nakufanya bao kuwa 2-1
1-1
Derby County Fc wamesawazisha bao kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko wakiwa nguvu sawa ya bao 1-1 na Manchester United. 
Rooney akishangilia bao lake dakika ya 16 kipindi cha kwanza.
George Thorne aliisawazishia bao Derby katika kipindi hicho hicho dakika ya 37 na kufanya bao kuwa 1-1.
Rooney Dakika ya 16 kapachika bao na Man United kutangulia kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Derby.
Mhh!! Wayne Rooney alionekana kama alikuwa Offside kabla ya kupata pasi na kufunga bao la kwanza
VIKOSI:
Derby County walioanza XI: Carson, Christie, Keogh, Martin, Shackell, Johnson, Butterfield, Blackman, Ince, Thorne, Warnock
Derby Akiba: Grant, Bryson, Hendrick, Russell, Baird, Camara, Olsson
Manchester United walioanza XI: De Gea, Varela, Smalling, Blind, Borthwick-Jackson, Fellaini, Schneiderlin, Mata, Lingard, Martial, Rooney
Man Utd Akiba: Romero, McNair, Carrick, Herrera, Januzaj, Pereira, Memphis
kushoto ni Wayne Rooney

Manchester United Ed Woodward akiwa tayari kwenye Uwanja wa iPro Stadium kushuhudia Timu ya Man United ikifungua Dimba la FA CUP raundi ya Nne.

Meneja wa Man United Louis Van Gaal akiwa kwenye Uwanja wa iPro usiku huu akitupia jicho kuona kama Timu yake itambeba leo hama vipi.

No comments:
Post a Comment