BUKOBA SPORTS

Thursday, January 28, 2016

CAPITAL ONE CUP: MANCHESTER CITY 3 v 1 EVERTON (Agg 4-3)


Manchester City wametinga Fainali ya C1C, Capital One Cup, baada ya kufungwa Mechi ya Kwanza 2-1 na Jana kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuishinda Everton 3-1.
Sasa Man City watacheza Fainali Uwanjani Wembley Jijini London dhidi ya Liverpool ambayo Juzi iliibwaga Stoke City kwa Penati 6-5 baada ya kutoka Sare ya 1-1 kwa Mechi mbili.
Jana, huko Etihad, City walijikuta wako nyuma 1-0 kwa Bao la Dakika ya 18 la Ross Barkley lakini wakasawazisha Dakika ya 24 kupitia Fernandinho na Kipindi cha Pili kuongeza Bao nyingine 2 Dakika za 70 na 76 kupitia Kevin de Bruyne na Sergio Aguero.
City sasa wamesonga Fainali kwa Jumla ya Mabao 4-3 kwa Mechi mbili.


Nusu Fainali-Kanuni Muhimu:
-Kwenye Mechi za Nusu Fainali, ikiwa Jumla ya Magoli kwa Mechi 2 ni sawa baada ya Dakika 90 za Mechi ya Marudiano, Nyongeza ya Dakika 30 itachezwa.
-Ikiwa Gemu ni Sare baada ya hiyo Nyongeza ya Dakika 30, Mshindi atapatikana kwa kuhesabu Goli la Ugenini kuwa mara mbili.
-Ikiwa Gemu bado itakuwa sawa hata baada ya kuhesabu Goli za Ugenini ni mara mbili, basi Mshindi atapatikana kwa Mikwaju ya Penati 5 kama Sheria za Soka zinavyotamka.

Etihad Stadium
Manchester City bao limefungwa na Fernandinho dakika ya 24
Everton bao limefungwa na Ross Barkley dakika ya 18

No comments:

Post a Comment