Diego akishangilia bao lake dakika ya 23
Diego Costa, ameacha gumzo kubwa baada ya kusababisha Sentahafu wa Arsenal apewe Kadi Nyekundu katika Dakika ya 18 na yeye kuifungia Chelsea Bao pekee na la ushindi katika Dakika ya 23.
Arsenal, wakiwa kwao Emirates, walipata balaa Dakika ya 18 tu baada ya Sentahafu wao, Per Mertesacker, kumwangusha Diego Costa aliekuwa akichanja mbuga kumuona Kipa na Refa Mark Clattenburg kuamua ni Kadi Nyekundu ingawa tukio hili limegawa pande kila Mtu akibaki na nini alichoona yeye.
Chelsea wanaongoza bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Arsenal bao likifungwa na Diego Costa dakika ya 23 kipindi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment