Arsenal Leo wametoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuwafunga Mtu 10 Leicester City Bao 2-1.
Ushindi huu umewafikisha Arsenal Pointi 51 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Leicester na sasa wako Nafasi ya Pili lakini wanaweza kushushwa baadae Leo ikiwa Tottenham itaifunga Man City huko Etihad.
Kipindi cha Pili Dakika ya 54, Leicester walibaki Mtu 10 baada ya Simpson kupewa Kadi ya Njano ya Pili kwa kumvuta Mkono Giroud na hivyo kuonyeshwa Kadi Nyekundu.
Dakika ya 70 Arsenal walisawazisha Bao kupitia Theo Walcott alieingia Dakika ya 60 kumbadili Coquelin.
Bao la ushindi kwa Arsenal lilifungwa na Danny Welbeck, Mchezaji ambae alikuwa Majeruhi tangu Aprili Mwaka Jana na kuingizwa Dakika ya 83 kumbadili Oxlade-Chamberlain, na kufunga Bao hilo muhimu katika Dakika ya 94 kwa Kichwa kufuatia Frikiki ya Mesut Ozil.
VIKOSI:
Arsenal walioanza XI: Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Ozil, Sanchez, Giroud
Arsenal Akiba: Ospina, Walcott, Flamini, Chambers, Welbeck, Campbell, Elneny
Leicester City starting XI: Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Mahrez, Drinkwater, Kante, Albrighton, Okazaki, Vardy
Leicester AkibaKing, Gray, Ulloa, Dyer, Wasilewski, Chilwell, Schwarzer
No comments:
Post a Comment